1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na Lebanon zasitisha mapigano

17 Aprili 2026

Makubaliano ya siku 10 ya kusitishwa mapigano kati ya Lebanon na Israel yameanza Ijumaa.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Ohad Zwigenberg/AP Photo/picture alliance

Haya yanakuja wakati ambapo Rais Donald Trump wa Marekani amesema anajaribu kupanga mkutano wa kwanza kabisa wa ana kwa ana kati ya viongozi wa mataifa hayo mawili.

Makubaliano hayo ya kusitishwa mapigano ambayo Trump alikuwa amesema yataanza kutekelezwa saa sita usiku kwa saa za Lebanon na Israel, yanakuja huku Marekani ikiwa inaongeza juhudi za kufikia mkataba wa kusitisha vita na Iran, huku Tehran ikisisitiza kusitishwa vita Lebanon ni lazima kuwe sehemu ya makubaliano yoyote yale.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonyesha kufurahia makubaliano hayo na kutoa wito wa pande zote mbili kuyaheshimu makubaliano hayo.

Trump vile vile amesema Washington iko "karibu mno" kufikia mkataba wa amani na Iran baada ya wiki sita za vita na huenda akasafiri kuelekea Pakistan kusaini mkataba wowote wa amani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW