Israel na Palestina wako tayari kubadilishana wafungwa.
9 Aprili 2007Ujumbe huo umeleta hali ya msisimko katika maeneo ya Jerusalem , Jafar, Ramallah na miji mingine , ambayo Wakristo walikuwa wakisherehekea sikukuu ya Pasaka siku ya Jumapili. Majadiliano juu ya kuchiliwa huru kwa mwanajeshi wa Israel aliyetekwa nyara Gilad Schalit yamepiga hatua. Ghasi hamad, msemaji wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina , alifafanua kuwa majadiliano juu ya mabadilishano ya wafungwa yamepiga hatua kubwa. Wajumbe wa majadiliano kutoka upande wa Israel na Palestina pamoja na wapatanishi kutoka Misr wamefikia maafikiano, ya kwamba ni wafungwa wangapi wa Palestina watabadilishwa na mfungwa mmoja mwanajeshi wa Israel Schalit.
Pia katika suala la ni wafungwa wa aina gani ambao wataachiwa limepata muafaka.
Kwa upande wa kundi la majadiliano la Wapalestina katika majadiliano hayo limeeleza kuwa Israel wameangalia suala la wafungwa watakaowaachilia huru, ambao kama wanavyosema kuwa ni wale ambao mikono yao haina damu.
Pia wale ambao wamekuwapo kifungoni kwa muda mrefu, ambao tayari walikuwa kifungoni kabla ya kutiwa saini kwa makubaliano ya mjini Oslo katika mwaka 1993, pia hawa wataachiwa.
Pia suala kuhusiana na kuchiliwa huru kwa Marwan Barguti mwanasiasa maarufu wa Kipalestina kutoka chama cha Fatah lilizungumziwa. Waziri mpya wa habari wa serikali ya Palestina Mustafa Barguti anaeleza kuwa,
upande wa Palestina umeonyesha unyumbulifu mkubwa kuhusiana na suala hili la Schalit. Umejibu ombi la jumuiya ya kimataifa na kutoa kwa Israel majina ya wafungwa wa Kipalestina ambao wanapaswa kuachiliwa huru kwa kubadilishana na Schalit. Mpira sasa uko upande wa Israel.
Kwa upande mwingine anadhibitisha mwakilishi wa Israel, kuwa hatua zimepigwa katika majadiliano hayo. Pamoja na hayo anasema kuwa njia ya kuelekea katika kuachiliwa huru kwa wafungwa hao bado ni ndefu. Amewaonya hata hivyo Wapalestina dhidi ya kuwa na matarajio makubwa. Israel iko tayari, hata wafungwa ambao wanahusika na mauaji kadha kuwaacha huru, lakini sio wafungwa ambao ni viongozi.
Mwanajeshi wa Israel Gilad Schalit, amejikuta tangu Juni 25 mwaka jana akiwa ameanzisha mapambano dhidi ya Palestina. Wakati huo alikuwa na umri wa miaka 19. Makundi matatu ya wapiganaji wa Kipalestina waliingia katika kituo cha kijeshi cha Israel karibu na ukanda wa Gaza na kumkamata Schalit na kumpeleka Gaza.