Netanyahu: Kuna hatua katika kuwarejesha mateka.
21 Novemba 2023![Israel-Hamas War 2023: Netanyahu Visits Gaza Border](https://static.dw.com/image/67410291_800.webp)
Matangazo
Hatua hiyo ni baada ya wapatanishi wa Qatar na Kiongozi wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh kusema kuwa makubaliano hayo yanakaribia. Raia wa Palestina wana matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano hayo. Kulingana na makubaliano hayo, Hamas itaawachilia mateka kati ya 50 na 100 huku Israel ikiwaachilia huru Wapalestina wapatao 300 na kusitisha mapigano kwa muda wa siku tano.