1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yapokea miili ya mateka zaidi kutoka Gaza

15 Oktoba 2025

Jeshi la Israel limepokea mabaki ya mateka wanne waliokabidhiwa na Hamas chini ya mpango wa kusitisha mapigano. Wakati huo huo, hospitali ya Gaza imethibitisha kupokea miili ya Wapalestina 45 waliorejeshwa na Israel

Israeli Kfar Maas 2025 | Mazishi ya mateka wa Kiaisraeli Idan Shtivi
Mazishi ya mateka wa Kiaisraeli Idan ShtiviPicha: Maya Levin/AFP/Getty Images

Jeshi la Israel limesema limepokea mabaki ya mateka wanne waliokabidhiwa na Hamas Jumanne, katika hatua nyingine ya utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Rais wa Marekani Donald Trump. Miili hiyo ilikabidhiwa kwa Msalaba Mwekundu kabla ya kupelekwa Israel kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu.

Siku moja kabla, Hamas ilikuwa imekabidhi mabaki ya mateka wanne wengine, saa chache baada ya kuachilia mateka 20 walio hai chini ya makubaliano hayo ya amani. Jeshi la Israel lilisema makubaliano hayo ni sehemu ya mpango mpana wa kurejesha amani na kumaliza vita vya miaka miwili katika Ukanda wa Gaza.

Hospitali ya Nasser mjini Khan Younis imepokea miili ya wafungwa 45 wa Kipalestina waliokabidhiwa na israel.Picha: Alaa Abo Mohsen/APA Images/ZUMA/picture alliance

Miili ya mateka wa Kipalestina yakabidhiwa pia

Wakati huo huo, hospitali ya Nasser Medical Centre huko Gaza imesema imepokea miili ya Wapalestina 45 waliokuwa wakihifadhiwa na Israel. Kulingana na mpango huo, Israel inatakiwa kurejesha miili ya Wapalestina 15 kwa kila Mwizraeli aliyefariki vitani.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema serikali yake itaendelea na juhudi za kuhakikisha "mateka wote wanarudi nyumbani,” huku familia zikisubiri kwa wasiwasi. Rais Trump kupitia mtandao wa X alisema, "Mzigo mkubwa umeondoka, lakini kazi haijaisha — awamu ya pili inaanza sasa.”

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW