1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Israel yarusha kombora katika makazi ya kiongozi wa Hamas

Angela Mdungu
4 Novemba 2023

Jeshi la Israel limeshambulia kwa ndege isiyokuwa na rubani nyumba ya kiongozi wa kundi la Hamas Ismail Haniye iliyopo katika Ukanda wa Gaza.

Israel Gaza | Angriff auf den Gazastreifen in Khan Younis
Mkazi wa Gaza akiangalia uharibifu wa jengo baada ya shambulizi la Israel: 03.11.2023Picha: Fatima Shbair/AP Photo/picture alliance

Taarifa iliyotolewa leo na redio yenye mfungamano na kundi hilo ya Al Aqsa imesema kuwa haifahamiki ikiwa kulikuwa na mwanafamilia yoyote wa kiongozi huyo wakati wa shambulio hilo.

Haniye hata hivyo yuko nje ya Ukanda wa Gaza tangu mwaka 2019 ambapo amekuwa akiishi kati ya Uturuki na Qatar.

Katika hatua nyingine, Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Anthony Blinken leo atakutana nchini Jordan na mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa ya Mashariki ya kati, katika juhudi za kusaidia  kusitisha mapigano huko Gaza.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Jordan imesema viongozi hao wataelezea msimamo wa nchi za Kiarabu wa kutaka kusitishwa kwa mapigano haraka na kuwasilishwa kwa misaada ya kibinaadamu. Kabla ya kuanza kwa mkutano huo, Blinken amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Jordan Najib Mikati aliyesisitiza umuhimu wa kufanya juhudi za kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW