1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel tayari kupatanisha mzozo wa Urusi na Ukraine

1 Februari 2023

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema anafikiria kuhusu msaada wa kijeshi kwa Ukraine na yupo tayari kuwa mpatanishi kwenye mzozo huo, kufuatia wito wa Marekani kwa Israel kuhusika zaidi.

Israels Premierminister Netanjahu
Picha: Menahem Kahana/AFP POOL/AP/dpa/picture alliance

Netanyahu alisema hayo kwenye mahojiano yaliyorushwa siku ya Jumanne (Januari 31, lakini hakutoa ahadi madhubuti kwa Ukraine.

Israel imehifadhi uhusiano wake na Urusi, ambayo inadhibiti anga ya taifa jirani la Syria, nayo Urusi imefumbia macho mashambulizi ya angani yanayofanywa na Israel dhidi ya Iran, mshirika muhimu wa Moscow kwenye eneo la Mashirika ya Kati.

Kwenye mahojiano hayo na kituo cha televisheni cha CNN cha Marekani, Netanyahu aliulizwa ikiwa angelitoa msaada kama vile mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora chapa Iron Dome kwa Ukraine, naye akajibu kwa kusema angali anatafakari kuhusu hilo.

Mfumo huo wa kiteknolojia unaoungwa mkono na Marekani huilinda Israel dhidi ya mashambulizi ya kutokea angani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW