1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel: Tumesikitishwa na shambulizi lenye madhara Gaza

29 Desemba 2023

Jeshi la Israel limedai kusikitishwa na kile lilichokiita kuwa tukio lenye "madhara kwa watu wasiohusika" baada ya shambulizi lake la hivi majuzi kwenye kambi ya wakimbizi ya al-Maghazi katikati mwa Ukanda wa Gaza.

Ukanda wa Gaza | Eneo la Gaza lililoathiriwa na mashambulizi yanayoendelea ya Israel
Eneo la Gaza lililoathiriwa na mashambulizi yanayoendelea ya IsraelPicha: Mohammed Talatene/dpa/picture alliance

Eylon Levy, msemaji wa serikali ya Israelamesema hilo ni kosa la kusikitisha na halikupaswa kutokea na kuongeza kuwa mkakati wao ni kupunguza vifo vya raia huku wakiwashutumu Hamas kutoheshimu hilo.

"Tunasikitika kuona watu wamepoteza maisha kwa sababu tunajaribu kufanya kila tuliwezalo ili kupunguza vifo vya raia wakati Hamas wana mkakati wa kuviongeza. Tunaendelea kujifunza na kuzidisha juhudi zetu za kuwaweka raia eneo salama." Alisema Levy.

Soma pia:Matukio yanayoendelea katika vita vya Israel-Hamas

Wizara ya Afya inayodhibitiwa na Hamas ilisema kuwa zaidi ya watu 70 waliuawa wakiwemo watoto huku maafisa wa Umoja wa Mataifa wakibaini kuwa watu 86 waliuawa.

Shambulio hilo la Desemba 24 lilifanywa kwenye kambi yaal-Maghazi wanakoishi wakimbizi wapatao 33,000.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW