1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel: Utambuzi wa taifa la Palestina ni 'tuzo kwa ugaidi'

10 Aprili 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Gideon Saar amelishtumu tangazo la Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kwamba nchi yake inaweza kulitambua taifa la Palestina ifikapo mwezi Juni.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron akihutubia waandishi wa habari baada ya mkutano wa "coalition of the willing" katika ikulu ya Elysee mjini Paris mnamo Mchi 27,2025
Rais wa Ufaransa, Emmanuel MacronPicha: Ludovic Marin/Pool/REUTERS

Katika taarifa yake kwenye mtandao wa kijamii wa X jana jioni, Saar alisema kutambuliwa kwa upande mmoja kwa taifa la Palestina na nchi yoyote ile, hakutaleta amani, usalama na utulivu katika kanda hiyo, lakini kinyume chake itawasukuma mbali zaidi.

Macron asema Ufaransa inapanga kulitambua taifa la Palestina

Jumatano, Rais Macron alisema kuwa Ufaransa inapanga kulitambua taifa la Palestina ndani ya miezi kadhaa na huenda ikachukuwa hatua hiyo wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini New York mwezi Juni.

Rais huyo ameongeza kuwa lengo lao ni kuongoza mkutano huo na Saudi Arabia mwezi Juni, ambapo wanaweza kukamilisha mchakato huo wa kutambuliwa na mataifa kadhaa.

    

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW