1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaahidi "kufungua kwa sehemu" kivuko cha Rafah

26 Januari 2026

Israel imetangaza leo alfajiri kuwa itaruhusu "kufunguliwa kwa sehemu" kivuko muhimu cha mpakani cha Rafah kilichopo baina ya Misri na Ukanda wa Gaza

Misri Rafah 2025 | Kivuko cha Rafah
Kivuko cha RafahPicha: Mohammed Arafat/AP Photo/dpa/picture alliance

Hata hpale itakapoyapata mabaki ya mateka wake wa mwisho inayeaminika amezikwa kwenye ardhi hiyo ya Wapalestina.

Kufunguliwa kwa kivuko hicho -- ambacho ni lango muhimu la upelekaji misaada ya kiutu ndani ya Ukanda wa Gaza-- ilikuwa sehemu ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyosimamiwa na Marekani Oktoba mwaka jana.

Hata hivyo, Israel iliendelea kukifunga licha ya shinikizo kubwa la kimataifa. Mnamo mwishoni mwa juma, wawakilishi wa Marekani walifanya ziara nchini Israel na kuarifu kwamba wameishinikiza serikali ya nchi hiyo kukifungua kivuko hicho.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imesema Israel imeridhia kuchukua hatua hiyo pale wanajeshi wake watakapokamilisha oparesheni ya kuutafuta mwili wa mateka pekee aliyebakia kwenye Ukanda wa Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW