Israel yaamua kuwaachia huru wafungwa 90 wa kiipalastina
23 Septemba 2007Matangazo
Jerusalem:
Serikali ya Israel imeamua kuwaachia huru wafungwa 90 wa kipalastina.Uamuzi huo unaangaliwa kama hatua ya kumuunga mkono rais wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas.Wafungwa hao wanaoachiwa huru ni wanachama wa Fatah.Jumla ya wapalastina elfu kumi na mmoja wanashikiliwa korokoroni nchini Israel.