1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yaanza operesheni mpya katika Ukingo wa Magharibi

26 Novemba 2025

Jeshi la Israel limetangaza operesheni mpya lililoitaja kuwa y kupambana na ugaidi" kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya jeshi na Shirika la Ujasusi la Ndani la taifa hilo.

Israel imeanzisha operesheni ya "kupambana na ugaidi"Ukingo wa Magharibi
Wanajeshi wa Israel wakimkamata mkaazi wa kambi ya wakimbizi ya Nur Shams katika Ukingo wa MagharibiPicha: Zain Jaafar/AFP

Israel imesema hata hivyo operesheni hiyo ni mpya na si sehemu ya ile iliyoanzishwa Januari inayozilenga kambi za wakimbizi wa Kipalestina.

Mshambulizi kwenye Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu na Israel tangu mwaka 1967 yameongezeka tangu wanamgambo wa Hamas walipoishambulia Israel na kuibua vita Oktoba 7, 2023.

Israel yatambua mabaki ya mateka mwingine yaliyorejeshwa nyumbani

Wakati huo huo, Israel imeyatambua mabaki ya mateka wa hivi karibuni zaidi kurejeshwa nyumbani kutoka Ukanda wa Gaza kuwa ni ya Dror Or, mwanamume aliyeuawa Oktoba 7, 2023 katika eneo la Kibbutz Be'eri, na mwili wake ulipelekwa Gaza. Kurejeshwa kwa mabaki ya Or ni sehemu ya makubaliano ya kusitisha vita kati ya Israel na Hamas yanayojumuisha kubadilishana mateka walio hai na wafu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW