1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yadai kumuua Kiongozi wa kundi la Islamic Jihad

5 Mei 2024

Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kipalestina wa Islamic Jihad ameuawa katika shambulizi la anga kusini mwa Gaza.

Shambulio katika Kambi ya Nour Shams katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu
Moshi ukifuka baada ya shambulio la Israel katika kambi ya wakimbizi ya Nur Shams karibu na mji wa Tulkarem katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israel: 20.04.2024Picha: Majdi Mohammed/AP Photo/picture alliance

Hayo yameelezwa na Jeshi la Ulinzi la Israel IDF ambalo limesema kwamba Aiman Zaarab alikuwa mmoja wa makamanda wa kundi hilo huko Rafah na kuwa alihusika katika shambulio la Oktoba 7. Wanamgambo wengine wawili wa kundi hilo wameuawa pia katika shambulio hilo.

Soma pia: Netanyahu aapa kuushambulia mji wa Rafah

Wiki hii Israel iliifahamisha Marekani kuhusu mpango wa kuwahamisha raia wa Kipalestina kabla ya uwezekano wa kuanzisha operesheni ya kijeshi huko Rafah katika dhamira ya kulitokomeza kabisa kundi la Hamas. Watu wengine watano wameripotiwa kuuawa katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israel.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW