1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yadhamiria kujitanua eneo la Milima ya Golan

16 Desemba 2024

Serikali ya Israel imeidhinisha mpango wa kuongeza idadi ya watu kwenye eneo la Syria inalolikalia kwa mabavu la milima ya Golan.

Milima ya Golan
Milima ya GolanPicha: Tsafrir Abayov/AP/picture alliance

Serikali ya Israel imeidhinisha mpango wa kuongeza idadi ya watu kwenye eneo la Syria inalolikalia kwa mabavu la milima ya Golan. Serikali hiyo ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu imetoa ridhaa ya kutimika kiasi dola milioni 11 kwa mpango mpya wa kutanua makaazi ya Waisraeli kwenye milima ya Golan.

Ofisi ya Netanyahu imesema malengo ni kuongeza maradufu idadi ya Waisraeli 30,000 wanaoishi sasa kutokana na umuhimu wa eneo hilo kwa usalama na maslahi ya Israel. Israel ililikamata eneo hilo la mwinuko tangu baada ya vita vya siku sita kati yake na mataifa ya kiarabu vya mnamo 1967 na kisha kulitwaa kwa nguvu mwaka 1981.

Ukaliaji huo hautambuliwi chini ya sheria za kimataifa na ni Marekani pekee ndiyo ilitambua uhalali wa Israel kulithibiti eneo hilo.

Tangazo hilo la Israel limezusha ukosoaji kutoka mataifa kadhaa ya kiarabu ikiwemo Saudi Arabia na Qatar ambayo yamesema ni ukiukwaji mwingine wa wazi wa sheria ya kimataifa unaofanywa na Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW