1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaendelea kuishambulia Iran

3 Machi 2026

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi mapya usiku wa kuamkia leo dhidi ya kile imekitaja kuwa "utawala wa kigaidi wa Iran" kwenye mji mkuu Tehran, ikililenga jengo la shirika la utangazaji la nchi hiyo IRIB.

Iran Tehran 2026 | Athari za mashambulizi ya Israel kwenye mji mkuu wa Iran, Tehran
Athari za mashambulizi ya Israel kwenye mji mkuu wa Iran, Tehran.

Vishindo vya makombora vilisika mnamo usiku wa kuamkia leo mjini Tehran na kituo cha telesheni nchini Iran cha Press TV kiliripoti makao makuu ya IRIB yalishambuliwa.

Mashambulizi hayo ni mwendelezo wa hujuma nzito za kijeshi zilizofanywa kutwa nzima jana Jumatatu na vikosi vya Israel nchini Iran. Rais Donald Trump wa Marekani aliwaambia waandishi habari mjini Washington kwamba vita hivyo vinaweza kuendelea kwa muda wa wiki tano na zaidi.

Utawala wake umeionya Iran kujiandaa kwa mashambulizi makubwa zaidi yatakayoisambaratisha miundombinu ya kijeshi ya nchi hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW