1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yazidi kushinikizwa kusitisha vita Gaza

18 Desemba 2023

Wizara ya afya huko Gaza imesema Israel imewaua watu 110 kaskazini mwa ukanda huo tangu siku ya Jumapili, wakati miito ikizidi kuhanikiza kwa taifa hilo kusitisha vita.

Gaza |Uharibifu wa vita yva Israel Gaza
Vita vya Israel-Hamas vimeharibu sehemu kubwa ya Ukanda wa GazaPicha: Mahmoud Sabbah/AA/picture alliance

Wakati miito ya usitishwaji mapigano ikiendelea kutolewa, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin anatazamiwa kufanya ziara hii leo huko Israel.

Ujerumani, Uingereza na Ufaransa zimetoa wito wa usitishwaji wa mapigano yatakayosababisha mateka zaidi kuachiliwa na kufanikisha uwasilishwaji wa misaada ya kibinaadamu katika Ukanda wa Gaza. 

Soma pia: Jeshi la Israel limegundua handaki kubwa zaidi linalotumiwa na Hamas

Shirika la Afya Duniani, WHO, limeelezea wasiwasi wake kuhusu uharibifu mkubwa katika hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Gaza. Leo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupigia kura azimio jipya la kutaka "kusitishwa kwa haraka mapigano" huko Gaza. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW