Israel yaendeleza mashambulizi Gaza na kuuwa watu 17
28 Novemba 2024Watu sita waliuauwa katika mashambulizi mawili tofauti ya angani kwenye nyumba moja na karibu na hospitali ya Kamal Adwan eneo la Beit Lahiya kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. Watu wengine wanne waliuwawa wakati wakati shambulizi la Israel liliipiga pikipiki katika eneo la Khan Younis kusini mwa Gaza.
Katika eneo la Nuseirat, mojawapo ya kambi nane za wakimbizi huko Gaza, ndege za Israel lilifanya mashambulizi kadhaa ya angani na kuharibu jengo la ghorofa kadhaa. Watu saba waliuawa kwenye mashambulizi hayo.
Hezbollah yatangaza "ushindi" dhidi ya Israel
Madaktari wamesema watu wawili, mwanamke na mtoto, waliuawa katika shambulizi lililofanywa na kifaru kwenye maeneo ya magharibi ya Nuseirat, wakati shambulizi ya angani liliuwa watu wengine watano katika nyumba iliyokuwa karibu.
Makubaliano yanaendelea kuzingatiwa juu ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hezbollah, mshirika wa Hamas nchini Lebanon, tangu yalipoanza kutekelezwa jana.