1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yaendeleza mashambulizi yake Gaza na Lebanon

9 Novemba 2024

Jeshi la anga la Israel limeshambulia ngome za kundi la Hamas kusini mwa mji mkuuu wa Lebabon, Beirut, huku jeshi la ardhini likiendelea na mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza.

Mgogoro wa Mashariki ya Kati
Israel yaendeleza mashambulizi yake Gaza na LebanonPicha: Mahmud Hams/AFP

Jeshi hilo limesema limelenga maeneo ya mawasiliano na ya kutengeneza silaha ya kundi hilo pamoja na miundombinu yao mjini Dahiyeh. 

Jeshi limesisitiza kuwa kabla ya operesheni hiyo kuanza, hatua kadhaa zilichukuliwa ili kuepuka kuwashambulia raia. 

70% ya waliouawa ukanda wa Gaza ni wanawake na watoto

Katika taarifa ya jeshi hilo iliyotumwa katika mtandao wa Telegram, shambulizi jengine lililofanywa na jeshi la ardhini limewauwa wanamgambo kadhaa katika kambi ya Jabalia kaskazini mwa Gaza. 

Israel ilianzisha kampeni yake dhidi ya kundi la Hamas Oktoba 7 mwaka 2023 baada ya kundi hilo kushambulia kusini mwa Israel na kusababisha vifo vya watu 1,200. Tangu Israel ianze mashambulizi hayo, Wapalestina zaidi ya 40,000 wameuwawa huku mamilioni kadhaa wakipoteza makaazi yao. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW