1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel yafanya mashambulizi ya anga dhidi ya Iran

26 Oktoba 2024

Jeshi la Iran limesema wanajeshi wake wawili waliuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya vituo vya kijeshi katika nchi hiyo leo Jumamosi.

Iran inasema Israel ilishambulia kambi zake za kijeshi
Iran inasema Israel ilishambulia kambi zake za kijeshiPicha: Vahid Salemi/AP Photo/picture alliance

Jeshi la Iran limesema mifumo ya ulinzi wa anga imekinga mashambulizi ya Israel kwa mafanikio, ingawa kumetokea "uharibifu mdogo" katika baadhi ya maeneo.

Israel imethibitisha kufanya "mashambulizi ya kulipiza kuzilenga ngome za kijeshi nchini Iran". Hapo awali Marekani iliionya Israel kutoshambulia maeneo ya nyuklia na mafuta ambayo yanaweza kuzua mzozo mkubwa katika eneo la Mashariki ya Kati.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, ameitaka Iran kutojibu mashambulizi ya Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW