1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafanya mashambulizi dhidi ya Lebanon

Eric Kalume Ponda8 Januari 2009

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita vya Gaza, mashambulizi ya mizinga ya kutoka ardhi ya Lebanon yameripotiwa kushambulia maeneo ya Kaskazini mwa Israel.

Israel yafanya mashambulizi ndani ya Lebanon.Picha: AP


Baada ya Israel kuanza kutekeleza mpango wa kusitisha mapigano kwa muda wa masaa matatu kila baada ya siku mbili, mashambulizi makali yameendelea katika eneo hilo la Gaza na sasa yanaonekana kusambaa hadi eneo la Kasuni mwa Lebanon.


Haliadhalika mashambulizi zaidi yanaripotiwa katika eneo la Gaza huku baraza la usalama la Umoja wa mataifa likionekana kugawanyika kuhusu m zozo huo wa Gaza.


Serikali ya Israel imesema kuwa watu wawili waliuawa kufatuatia shambulizi hilo la mizinga 4 ya roketi iniliyorushwa kutoka kutoka eneo la Kusini mwa Lebanon.

Mizinga ya Israel ilishambulia mji wa Nahariya kilomita 10 kutoka eneo la mpakani ambapo serikali ya Lebanon iimewataka wakaazi wa eneo hilo kukimbilie maeneo ya usalama.


Hili ni shambulizi la kwanza kutekelezwa kutoka ardhi ya Lebanon ingawa serikali ya Lebanon imedai kuwa haikuhusika na shambulizi hilo na huenda lilitekelezwa na wafuasi wa Hamas walioko katika eneo katika eneo.

Maafisa wa serikali ya Lebanon wamesema kuwa wanafanya kila juhudi kubainisha nani aliyehusika na shambulizi hilo, kwani hadi sasa hakuna kundi lolote lilnalodai kuhusika.


Hali hiyo imezua hofu kubwa kwamba mataifa hayo mawili mawasimu wa zamani huenda yanarejelea uhasama wao wa muda mrefu tangu kumalizika kwa vita baina ya wafuasi wa kundi la Hezbollah na Israel mwaka wa 2006.


Lebanon inasema kuwa imejitolea kudumisha mkataba ulioafikiwa baina ya nchi hizo mbili ambao uliongozwa na umoja wa mataifa kumaliza mzozo baina ya nchi hizo mbili mwaka wa 2006.


Haya ni mashambulizi ya kwanza kabisa kufanyika baina ya Israel na Lebanon tangu Israel ianzishe mashambulizi yake dhidi ya wafuasi wa Hamas huko Gaza.

Jeshi la Israel limekuwa katika hali ya tahadhari kuu dhidi ya uwezekano wowote wa mashambulizi kutoka kwa kundi la Hezbolla tangu vita hivyo vianze tarehe 27 mwezi disemba mwaka uliopita.


Kwa upande mwengine jeshi hilo, liliendeleza mashambulizi yake dhidi ya eneo muhimu linaloaminika kuwa ngome ya wafuasi wa Hamas, baada ya muda wa masaa matatu uliotangazwa na Israel kumalizika.


Mashambulizi hayo yamekuwa yakiendelea usiku kucha baada ya Israel kushambulia kituo cha mkapani cha Raffa kwenye mpaka wa Gaza na Misri


Rais wa Israel Shimon Peres alisema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kuharibu njia zote zinazotumiwa na hamas kujipatia silaha huku akitoa onyo kali kwa Iran.

Shimon Peres akasema .``Malengo yetu hapa ni mawili. Kwanza hatuko tayarin kufungua vituo vya mpakani ili kutoa nafasi kwa Iran kuendelea kutuma silaha kwa Hamas. Hatungependa kuona Gaza ikitumiwa kama kituo cha Sattelite na Iran. Iran ndiyo inayotuma silaha hizi za mizinga ya roketi kwa Hamas kutushambulia. Na sasa hata wanataka kutuma mizinga ya roketi ya masafa marefu zaidi.. hilo haliwezekani. Pili ni kukomesha kabisa ugaidi sio tu kuuhalalisha´´.


Wakati huo huo juhudi za Umoja wa mataifa katika kuutanzua mzozo huo bado hazijapiga hatua baada ya wajumbe katika kikao cha hivi punde kuonekana kugawanyika kuhusiana na vita njia muafaka za kumaliza mzozo wa Gaza.


VIongozi kutoka matiafa ya kiarabu wanataka vita hivyo vikomeshwe na kuondoka kwa Israel huko Gaza, hali iliyonekana kutafautiana na Uingereza, Marekani na Ufaransa wanaotaka msimamo wa kadri utakaokubalika na pande zote mbili na hakikisho dhabiti la kwamba vituo vya mpakani kamwe havitatumiwa na wafuasi wa Hamasi kuingiza silaha haramu.








Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi