1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafanya mashambulizi katika wilaya moja Damascus

Sylvia Mwehozi
16 Novemba 2024

Vyombo vya habari vya umma nchini Syria vimeripoti kuwa Israel imefanya mashambulizi katika wilaya moja ya Mazzeh iliyoko katika mji mkuu wa Damascus siku ya Ijumaa.

Syria-Damascus
Jengo la makazi ya raia Syria lililoshambuliwa na mashambuizi ya IsraelPicha: LOUAI BESHARA/AFP via Getty Images

Vyombo vya habari vya umma nchini Syria vimeripoti kuwa Israel imefanya mashambulizi katika wilaya moja ya Mazzeh iliyoko katika mji mkuu wa Damascus siku ya Ijumaa. Makumi wauawa mashambulizi ya Israel huko Gaza, Lebanon na Syria

Wilaya hiyo ndiko kunapatikana majengo mengi ya balozi, makao makuu ya usalama na ofisi za Umoja wa Mataifa.

Shirika linalofuatilia haki za binadamu la Syria limesema kwamba mashambulizi hayo yalilenga maeneo ya kijeshi. Shirika hilo limeongeza kuwa watu 13, wakiwemo raia na wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran, waliuawa katika mashambulizi hayo.

Hayo yakiarifiwa, viongozi wa mataifa 20 yanayoongoza kiuchumi duniani watajumuika nchini Brazil siku ya Jumatatu katika mkutano wa kilele ambao utagubikwa na tofauti zilizopo kuhusu vita huko Mashariki ya Kati pamoja na Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW