1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafanya mashambulizi mapya Beirut

Josephat Charo
11 Machi 2026

Isael imefanya mashambulizi katika vitongoji vya kusini mwa mkuu wa Lebanon, Beirut. Jeshi la Israel linasema limeilenga tena miundombinu ya Hezbollah.

Mlipuko umezuka wakati Israel ilipokishambulia kijiji cha Abbasiyeh kusini mwa Lebanon
Mlipuko umezuka wakati Israel ilipokishambulia kijiji cha Abbasiyeh kusini mwa LebanonPicha: Kawnat Haju/AFP/Getty Images

Vyombo vya habari vya serikali ya Lebanon vimeripoti kwamba mashambulizi ya Israel yamevilenga vitongoji vya kusini mwa Beirut siku ya Jumatano, huku jeshi la Israeli likisema linalilenga tena kundi la wanamgambo wa Hezbollah linaloungwa mkono na Iran.

Shirika la Habari la Kitaifa la Lebanon linaloendeshwa na serikali limesema adui Israel ameanzisha uvamizi mkali katika vitongoji vya kusini mwa Beirut, ambako Hezbollah inatawala.

Kanda za moja kwa moja za televisheni ya AFP zilionyesha moshi mwingi ukifuka na kupaa angani kutoka maeneo yaliyoshambuliwa.

Jeshi la Israeli lilisema katika taarifa kwamba limeanza mashambulizi dhidi ya miundombinu ya Hezbollah katika eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW