1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafanya operesheni mpya ya kijeshi Khan Younis

9 Agosti 2024

Jeshi la Israel limefanya operesheni mpya ya kijeshi katika eneo la Khan Younis kusini mwa ukanda wa Gaza.

Gazastreifen Chan Junis | Palästinenser kehren zurück
Picha: Hatem Khaled/REUTERS/REUTERS

Taarifa za kijasusi zimeeleza uwepo wa wapiganaji katika eneo hilo na kwamba wamejipanga upya baada ya jeshi la Israel kuondoka katika eneo hilo.

Jeshi la Israel limefanya pia mashambulizi ya anga yaliyolenga zaidi ya shabaha 30 zenye mafungamano na kundi la wanamgambo la Hamas ikiwemo maghala ya silaha. Jeshi hilo limeongeza kuwa, wapiganaji kadhaa wa Hamas wameuawa katika mashambulizi hayo.

Israel ilifanya oparesheni kubwa ya kijeshi katika mji wa Khan Younis mwezi Julai japo wanajeshi wake waliondoka mwishoni mwa mwezi huo. Kulingana na ofisi ya mawasiliano inayodhibitiwa na Hamas, watu 255 waliuawa na wengine 300 walijeruhiwa wakati wa oparesheni hiyo ya jeshi la Israel katika eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW