Israel yafungua ubalozi wake Abu Dhabi
29 Juni 2021Lapid aliwasili kwenye Umoja wa Flame za Kiarabu (UAE) mapema Jumanne,akiwa afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Isreal kutembelea taifa hilo la Ghuba.
'' Israel inataka amani na majirani zake. Na majirani zake wote. Hatuendi popote. Mashariki ya Kati ndio kwetu. Tutasalia hapa'', alisema Lapid kwenye hafla hiyo ya uzinduzi ambayo ilihuzuriwa na waziri wa utamaduni na vijana wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Noura al-Kaabi na maafisa wengine wengi wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Isreal.
''Tunazitolea mwito nchi zote za kanda hili kufahamu hilo na kuja kuzungumza nasi'' aliondelea kusema.
Israel ilitia saini septemba mwaka jana mkataba ujiliakanao kama '' Abraham Accords'' uliorejesha mahusiano ya kidiplomasia na UAE pamoja Bahrain kufuatia upatanishi wa Mrekani.
'' Siyo mwisho wa barabara bali mwanzo wake''
Nchi hizo zimekuwa za kwanza kwenye eneo la Ghuba kurejesha mahusiano na Isreal, kinyume na misimiamo ya miongo kadhaa ya nchi za kiarabu kukataa kuweko na mahusiano na Israel hadi mzozo na palestina utapewa ufumbuzi.
''Tunachokifanya hapa leo siyo mwisho wa barabara bali mwanzo wake'' alisema Lapid.
Wakati waziara yake hiyo ya siku mbili,Lapid ametarajiwa kukutana na mwenzake waziri wa mamabo ya nje wa UAE, Abdullah bin Zayed al Nahyan. Anapanga kuzindua pia ubalozi mdogo wa Isreal mjini Dubai.
Mda mfupi baada ya kuwasili mjini Abu Dhabi, lapid aliandika kwenye ukarasa wake wa twitter kuwa anajivunia kuwakilisha taifa la Israel kwenye ziara hiyo rasmi ya kwanza kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu.