1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaharibu roketi iliyorushwa kutoka Lebanon

6 Aprili 2023

Jeshi la Israel limesema leo kuwa roketi iliyorushwa kutoka Lebanon hadi kwenye ardhi yake imenaswa na kuharibiwa.

Raketenfeuer aus dem Libanon auf Israel abgefeuert
Picha: Oren Ziv/AFP

Jeshi la Israel limesema leo kuwa roketi iliyorushwa kutoka Lebanon hadi kwenye ardhi yake imenaswa na kuharibiwa. Vyanzo vya usalama nchini Lebanon viliripoti kufanyika kwa mashambulizi hayo. 

Muda mfupi baadaye, Israel ilijibu mashambulizi kwa kufyatua mizinga kusini mwa Lebanon. Hakukuwa na taarifa kutoka kwa jeshi la Beirut au Jeshi la mpito la Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL).Israel na Lebanon zakubaliana mipaka ya baharini

Hayo yanajiri wakati mvutano ukioongezeka baada ya Israel wiki hii, kuvamia eneo la Msikiti wa Al-Aqsa huko Jerusalem huku wanamgambo wa Kipalestina wakirusha makombora kutoka Gaza kuelekea Israel.

Mapigano hayo yamezusha hofu ya kutokea mvutano mkubwa zaidi, wakati Waislamu wakiadhimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na Wayahudi wakijiandaa kwa Siku kuu ya Pasaka. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW