1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaishambulia Gaza

27 Januari 2023

Israel imeanzisha mashambulizi ya anga katika Ukanda wa Gaza leo, ikiwa ni katika kujibu shambulizi la roketi la wanamgambo lililorushwa kutoka eneo la Palestina.

Gaza | Israelische Luftangriffe auf Gaza
Picha: Arafat Barbakh/REUTERS

Taarifa ya jeshi imeeleza kuwa vikosi vya Ulinzi vya Israel kwa sasa vinashambulia katika Ukanda wa Gaza.

Duru za kiusalama za Gaza eneo linalodhibitiwa na kundi lenye itikadi kali za Kiislamu la Hamas, zimeeleza kwamba pamekuwepo na mashambulizi 15 yanayoyalenga maeneo ya wanamgambo, na hakuna majeruhi wowote walioripotiwa.

Soma zaidi: 

Nchi za kiarabu zaahidi kuendelea kuiunga mkono Palestina

Jeshi la Israel limesema mashambulizi ya awali ya roketi yalirushwa kutoka Gaza kuelekea Israel majira ya usiku.

Muda mfupi baada ya Israel kuanzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi saa kadhaa baadae, maroketi mengine matatu yalirushwa kutoka Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa jeshi, maroketi mengi kutoka Gaza yalizuiwa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW