1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yakosoa kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini ICJ

17 Mei 2024

Israel imeikosoa kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini kwenye Mahakama ya Haki ya Kimataifa, ICJ na kuitaja kuwa isiyo na uhalisia.

Majaji katika mahakama ya kimataifa ya haki ICJ
Majaji katika mahakama ya kimataifa ya haki ICJPicha: Peter Dejong/AP Photo/picture alliance

Israel leo imeikosoa kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini kwenye Mahakama ya Haki ya Kimataifa, ICJ na kuitaja kuwa isiyo na uhalisia wakati Afrika Kusini ikiwatolea wito majaji kuamuru kusitishwa kwa mapigano katika ukanda wa Gaza.

Wakili mkuu wa Israel katika kesi hiyo Gilad Noam, ameiambia mahakama hiyo kwamba Afrika Kusini inawasilisha ombi hilo kwa mara ya nne yenye taswira isiyo na uhalisia kuhusu kile kinachoendelea katika eneo la mzozo.

Akiizungumzia Israel, Zane Dangor, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano katika wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini amesema:

"Hii sasa ni mara ya tatu wanakuja kuomba amri ya muda. Na tunaomba amri ya muda kwa sababu hali katika eneo lote la Gaza na hasa Rafah imebadilika sana tangu mara ya mwisho tulipokuja mahakamani. Tunachokiona ni kuongezeka kwa mauaji ya kimbari .

Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant jana alisema kuwa operesheni huko Rafah itaendelea wakati wanajeshi wa nyongeza wakipelekwa kwenye eneo hilo.