1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel yakubali ujumbe wa UN kutathmini hali ya Gaza

10 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema Israel imekubali kupelekwa kwa mpango wa Umoja wa Mataifa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwa mjini Tel-Aviv:24.12.2023Picha: Ohad Zwigenberg/AP/dpa/picture alliance

Mpango huo utatakiwa kutathmini hali ilivyo eneo hilo, lengo ikiwa ni kuandaa mikakati ya kuwarejesha salama raia wa Gaza walioyakimbia makazi yao.

Hata hivyo Blinken amemsihi Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwapunguzia masaibu raia wa Gaza ambao amesema wanakabiliwa na madhila makubwa. Kulingana na wizara ya afya huko Gaza inayodhibitiwa na Hamas, zaidi ya watu 23,000 wameuawa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tel-Aviv, Blinken amesisitiza kuwa Wapalestina lazima waruhusiwe kurejea nyumbani mara tu hali itakaporuhusu na kwamba Marekani inapinga kabisa mapendekezo yoyote yanataka kuhamishwa kwa Wapalestina nje ya Gaza.