1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yalaani azimio la usitishwaji mapigano la UN

26 Machi 2024

Israel na Hamas zimeendelea kushikilia misimamo yao kuhusu usitishaji wa vita Gaza, baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kutaka vita hivyo visitishwe mara moja.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Maya Alleruzzo/AP/dpa/picture alliance

Hamas imelikataa pendekezo la hivi karibuni lililowasilishwa na wapatanishi wa kimataifa la usitishwaji wa mapigano na kuachiwa kwa mateka, wakati ambapo Israel imelilaani azimio la Umoja wa Mataifa lililotoa wito wa yote hayo kufanyika.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana hatimaye lilipitisha azimio hilo huku Marekani ikijiondoa katika kupiga kura jambo lililoighadhabisha Israel iliyotaka Marekani ipinge kwa kura ya turufu. Azimio hilo la Umoja wa Mataifa linatoa wito wa kuachiwa kwa mateka wote walioshikiliwa Gaza ila halitoi masharti ya kusimamishwa mapigano.

Kwa mara ya kwanza Baraza la Usalama la UN lilipitisha azimio kuhusu vita vya GazaPicha: Lev Radin/Sipa USA/picture alliance

Soma pia: Israel yakasirishwa na uamuzi wa Marekani kujizuwia na kura kuhusu azimio la Gaza

Hamas imesema kwamba itawashikilia mateka hadi pale Israel itakapokubali usitishwaji wa kudumu wa mapigano. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa upande wake anasema Israel inaweza kuyatimiza malengo yake ya kulisambaratisha kundi la Hamas na kuwaokoa mateka, iwapo watatanua mashambulizi yao ya ardhini hadi mji wa kusini wa Rafah.

Lakini waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock kwa mara nyengine ametoa wito kwa Israel kutofanya mashambulizi katika mji huo wa Rafah.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW