1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yalaumiwa na kamisheni ya haki za binaadam ya umoja wa mataifa

15 Aprili 2005

Geneva / Nablus:

Kamisheni ya haki za binaadam ya Umoja wa mataifa imeilaani kwa mara nyengine tena Israel kwa kutoheshimu haki za binaadam katika maeneo ya wapalastina.Azimio lililopitishwa na kamisheni hiyo mjini Geneva limelaani kile kilichotajwa kua "mauwaji yasiyoambatana na sheria,ujenzi wa ukuta pamoja na matumizi ya nguvu ya Israel dhidi ya umma wa Palastina.Nchi 29 zanachama zimeunga mkono azimio hilo,kumi,ikiwemo Ujerumani na Marekani zimepinga na 14 hazikuelemea upande wowote. Mataifa yaliyopinga yanalalamika, azimio hilo linaelemea upande mmoja tuu,halikulaani vimashambulio ya kigaidi.Katika maeneo ya utawala wa ndani kwenyewe,jeshi la Israel limempiga risasi na kumuuwa mwanaharakati wa kundi la wanamgambo wa Al Aqsa mjini Nablus.Viongozi wa utawala wa ndani wa palastina wamelaani mauwaji hayo ya makusudi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW