1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yamkosoa waziri wa ulinzi wa Pakistan kabla mkutano

Josephat Charo
10 Aprili 2026

Israel imeikosoa vikali Pakistan kabla ya mazungumzo yaliyopangwa kati ya Marekani na Iran kuhusu kuvifikisha mwisho kabisa vita kufuatia maoni ya waziri wa ulinzi wa Pakistani Khawaja Asif ya kuilaani Israeli.

Rais wa Marekani Donald Trump ana matumaini ya kupatikana makubaliano na Iran
Rais wa Marekani Donald Trump ana matumaini ya kupatikana makubaliano na IranPicha: Brendan Smialowski/AFP

Asif alikuwa ameielezea Israel kama ovu, laana kwa ubinadamu na taifa la saratani katika chapisho lake kwenye mtandao wa kijamii wa X Alhamisi, akiishutumu kwa kutekeleza mauaji katika Ukanda wa Gaza, Iran na Lebanon, na kusema anatumai wale waliohusika na kuunda dola hilo watateketezwa jehanamu.

Ofisi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu iliyaita matamshi ya Asif kuwa ya kuchukiza ikisema hakuna serikali inayopaswa kuvumilia matamshi kama hayo hasa ile inayofanya kazi kama mpatanishi asiyeegemea upande wowote.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema ana matumaini makubwa kuhusu uwezekano wa kufikia makubaliano na Iran kabla ya mazungumzo ya mwishoni mwa wiki hii mjini Islamabad, Pakistan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW