1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yamuuwa kamanda katika shambulizi Lebanon

17 Aprili 2024

Shambulizi la Israel limemuuwa kamanda mmoja wa Hezbollah kusini mwa Lebanon. Hayo yamesemwa na jeshi la Israel huku kundi hilo linaloungwa mkono na Iran likisema wanachama wake watatu waliuawa.

Ndege ya kivita ya Israel aina ya F15
Israel na wanamgambo wa Hezbollah wa Lebanon wamekuwa wakishambuliana tangu Hamas walipovamia Israel Oktoba 7Picha: Ariel Schalit/AP Photo/picture alliance

Jeshi la Israel limesema ndege yake ilishambulia na kumuuwa Ismail Yusef Baz, kamanda wa Hezbollah katika eneo la pwani, likiongeza kuwa  aliuawa katika eneo la kusini mwa Lebanon la Ain Baal.

Soma pia: Takriban watu saba waliuawa katika shambulizi la Israel nchini Lebanon.

Hezbollah imesema katika taarifa Baaz aliuawa, bila kutaja cheo chake wala jukumu lake. Israel na Hezbollah ambao ni washirika wa Hamas wamekuwa wakishambuliana kutokea pande zote za mpakani tangu kundi hilo la Kipalestina liliposhambulia kusini mwa Israel mnamo Oktoba 7, na kuzusha vita katika Ukanda wa Gaza.

Mshambulizi ya jana yamejiri huku mivutano ya kikanda ikiongezeka baada ya Iran kufanya shambulizi la makombora na droni dhidi ya Israel mwishoni mwa wiki kulipiza shambulizi kali la Israel lililofanywa kwenye ubalozi mdogo wa Tehran katika mji mkuu wa Syria, Damascus.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW