1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yapeleka polisi wengi eneo la maandamano

18 Mei 2023

Zaidi ya polisi 2,000 wamepelekwa kuwadhibiti Wayahudi wenye misimamo mikali wanaoandamana kupitia maeneo ya Wapalestina.

Israel | Die Zusammenstöße in Jerusalem
Picha: AHMAD GHARABLI/AFP/Getty Images

Maandamano hayo tete ya kuadhimisha kumbukumbu ya kutekwa kwa mji wa Jerusalem na vikosi vya Israel mnamo mwaka 1967, yanajiri mnamo wakati tayari kuna mzozo kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina.

Maafisa wamesema usalama ulioimarishwa ni juhudi za kuhakikisha hakuna vurugu zinatokea wakati wa maandamano hayo.

Yoram Segal, afisa mkuu wa polisi mjini Jerusalem aliwaambia waandishi habari hapo jana kwamba, polisi wamejitolea kuzuia machafuko wakati huu. Na ndiyo sababu takriban polisi 2,500 wamepelekwa eneo hilo kulinda usalama na kushughulikia kwa haraka tukio lolote la vurugu.

Polisi wameamua kuruhusu maelfu ya watu kuandamana kupitia Lango la Damascus la Jiji la Kale, licha ya ongezeko la ghasia za Israel na Palestina mwaka uliopita, na vilevile mapigano makali kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina katika ukanda wa Gaza wiki iliyopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW