1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yapokea mwili wa mateka mwingine wa Gaza

Josephat Charo
6 Novemba 2025

Israel imepokea mabaki ya mwili wa mateka mwingine wa Israel aliyekuwa akishikiliwa huko Gaza tangu shambulizi la Hamas mnamo Oktoba 7 mwaka 2023.

Israel imepokea mwili wa mateka wa Gaza kutoka kwa Shirika la Msalaba Mwekundu
Israel imepokea mwili wa mateka wa Gaza kutoka kwa Shirika la Msalaba MwekunduPicha: Abed Rahim Khatib/Anadolu Agency/IMAGO

Israel imepokea mwili wa mateka kutoka kwa shirika la Msalaba Mwekundu huko Gaza jana Jumatano, kulingana na ofisi ya waziri mkuu, katika makabidhiano ya hivi karibuni kufanyika chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Marekani.

Ofisi ya waziri mkuu ilisema katika taarifa kwamba jeneza la mateka huyo lilikabidhiwa kwa jeshi la Israeli na idara ya ndani ya usalama, na "litapokelewa kwa sherehe ya kijeshi" kabla ya kupelekwa katika kituo cha kitaifa cha uchunguzi wa kimahabara kwa ajili ya utambuzi.

Katika taarifa ya pamoja, jeshi na shirika la upelelezi wa ndani Shin Bet baadaye walithibitisha kwamba mabaki hayo yalivuka mpaka na kuingia katika dola ya Israeli", huku jeshi likiwahimiza umma kusubiri uthibitisho rasmi wa utambulisho wa marehemu.

Mwanzoni mwa makubaliano ya kusitisha mapigano mwezi uliopita, Hamas iliwaachilia mateka wote 20 waliosalia waliokamatwa wakati wa shambulio lake dhidi ya Israeli mnamo Oktoba 7, 2023, ambalo lilisababisha vita vya Gaza.

Kwa kubadilishana, Israeli iliwaachilia mamia ya wafungwa wa Kipalestina waliokuwa chini ya ulinzi wake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW