1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasema imemuuwa mkuu wa usalama wa Iran Ali Larijani

17 Machi 2026

Waziri wa ulinzi wa Israel Israel Katz amesema,mkuu wa usalama wa Iran Larijani ameuwawa kwenye mashambulizi ya jeshi la Israel ya kuamkia Jumanne

Uharibifu wa mashambulio ya Israel na Marekani katika mji mkuu wa Iran Tehran
Uharibifu wa mashambulio ya Israel na Marekani katika mji mkuu wa Iran TehranPicha: Fatemeh Bahrami/Anadolu/picture alliance

Ripoti zilizochapishwa muda mfupi uliopita na shirika la habari la AP zimesema, mkuu wa usalama wa taifa wa Iran Ali Larijani ameuwawa. Shirika hilo limemnukuu waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz.Vita na ukandamizaji vyazidisha kiwewe kwa Wairan

Iran haijathibitisha ripoti hizo. Vyombo vya habari vya Israel awali viliripoti juu ya kulengwa kwa mkuu huyo wa usalama wa Iran lakini havikwenda umbali wa kuthibitisha mara moja juu ya kuuliwa kwake.Jeshi la Israel limetangaza kuanzisha mashambulio mapya ikiyalenga maeneo mbali mbali ya miji ya Tehran na Beirut. 

Kwa upande mwingine mashambulizi ya droni na makombora ya Iran dhidi ya Umoja wa Falme za Kiarabu yamesababisha mripuko kwenye tenki ya mafuta katika eneo la pwani la mashariki mwa nchi hiyo linalopakana na Oman.Vita vya Marekani-Israel na Iran

Taarifa za kushambuliwa kwa mara nyingine eneo la Fujairah, zimekuja baada ya UAE kufunga kwa muda anga yake kufuatia vitisho mashambulio ya  Iran.

Vita hivyo vya Mashariki ya kati na Ghuba mpaka sasa vimesababisha mauaji ya watu 1,300 nchini Iran, takriban 850 Lebanon na watu 12 Israel kwa mujibu wa maafisa wa nchi hizo.

Jeshi la Marekani limesema wanajeshi wake 13 wameuwawa na wengine kiasi 200 wamejeruhiwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW