1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasema 'hatua zimepigwa' kusitisha mapigano Lebanon

11 Novemba 2024

Israel kupitia kwa waziri wake wa mambo ya nje, Gideon Saar, imeeleza kuwa kuna maendeleo fulani kuelekea usitishaji mapigano nchini Lebanon.

Israel inaendeleza mashambulizi Lebanon dhidi ya Hezbollah
Vita vimerindima kwa zaidi ya wiki sita nchini Lebanon wakati Israel ikiwalenga wapiganaji wa Hezbollah.Picha: Nidal Solh/AFP

Saar ametoa kauli hiyo mjini Jerusalem wakati alipoulizwa swali na waandishi wa habari, kuhusu uwezekano wa kusitishwa vita. Mwanadiplomasia huyo amejibu ya kwamba kuna hatua kadha zimepigwa na wanashirikiana na Marekani katika suala hilo.

Soma pia: Mashambulizi ya Israel yauwa zaidi ya watu 20 Lebanon

Hata hivyo, kundi la Hezbollah, limedai kwamba halijapokea mapendekezo yoyote kuhusu makubaliano ya usitishaji vita nchini Lebanon.

Msemaji wa kundi hilo, Mohammad Afif, ameeleza kwamba hadi kufikia sasa hakuna taarifa rasmi iliyowafikia lakini anaamini bado wamo katika hatua za kuwasalisha mapendekezo ya awali na majadiliano ya kina. Israel iliongeza mashambulizi ya anga mwishoni mwa mwezi Septemba yakilenga ngome za Hezbollah kote Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW