MigogoroIsrael
Israel yasema imefungua njia mpya kufikisha misaada Gaza
13 Aprili 2024Matangazo
Hata hivyo, Umoja wa Mataifa umesema kiwango cha misaada kinachoingizwa hakijamudu kupunguza madhila yanayowakabili Wapalestina kwa sababu ya changamoto za usambazaji zinazotokana na mapigano.
Miezi sita tangu kuanza kwa mapigano, zaidi ya watu milioni moja wanakabiliwa na kitisho cha baa la njaa hali inayozidisha mzozo wa kibinadamu kwenye Ukanda wa Gaza.
Mapambano kati ya vikosi vya Israel na wanamgambo wa Kipalestina bado yanaendelea bila ya kuwepo dalili ya kupatikana mkataba wa kusitisha mapigano.
Hapo jana, vikosi vya Israel viliwapiga risasi na kuwaua Wapalestina wawili kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi na walowezi wa Kiyahudi walivamia vijiji kadhaa wakachoma moto majengo na magari.