Israel yasema imeruhusu msaada zaidi kuingia Gaza
20 Aprili 2024Aidha, paleti 144 za chakula zilidondoshwa kutokea angani, na malori mengine 700 yanasubiri nyuma ya kituo cha ukaguzi cha Kerem Shalom, tayari kuchukuliwa na mashirika ya msaada ya Umoja wa Mataifa ya kusambaza chakula.
Kutokana na janga la kibinadamu linalowatishia watu wa Gaza, Israel imekuwa ikikabiliwa na shinikizo kubwa kutoka washirika wake wa magharibi na Umoja wa Mataifa, kuitaka iruhusu haraka kuingizwa kwa shehena zaidi za msaada.
soma pia:UNRWA lasema hakuna mabadiliko makubwa kuhusu misaada inayoingia Gaza
Ingawa mashirika ya wahisani yametambua ongezeko la msaada unaoingia Gaza, yanasisitiza kuwa bado malori yanayoruhusiwa kuingia hayatoshi, na kulalamika kuwa mapigano yanayoendelea yanakwamisha usambazaji wa msaada unaowasilishwa.