1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasema imewauwa ''magaidi watatu'' Gaza

30 Januari 2026

Jeshi la Israel limesema leo kuwa limefanya mashambulizi ya usiku kucha dhidi ya wale ililowaita magaidi wanane katika mji wa Rafah kusini mwa Gaza na kuwauwa watatu kati yao.

Shambulizi la Israel
Shambulizi la jeshi la Israel Gaza mnamo Novemba 22, 2025 licha ya makubaliano ya amaniPicha: IMAGO/Anadolu Agency

Katika taarifa yake, jeshi hilo limesema limewatambua magaidi wanane walioibuka kutoka maficho ya chini ya ardhi na kwamba jeshi la anga liliwalenga na kuwauwa watatu.

Bila kutoa maelezo yoyote kuhusu utambulisho wa walengwa wake, limesema mashambulizi yalifanywa na maafisa wake wanaendelea kufanya msako katika eneo hilo ili "kuwaangamiza magaidi wote."

Jeshi hilo limeongeza kuwa vikosi vyake vitaendelea kusalia katika eneo hilo kulingana na makubaliano ya kusitisha mapigano na vitaendelea kufanya kazi ili kukabiliana na tishio lolote.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW