1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yasema imewauwa wapiganaji wa Hamas huko Gaza

28 Oktoba 2023

Jeshi la Israel limearifu leo kuwa limewauwa wapiganaji kadhaa wa Kundi la Hamas kwenye Ukanda wa Gaza na kuyashambulia kiasi maeneo 150 usiku wa kuamkia leo.

Moto ukiwaka Ukanda wa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel
Mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza usiku wa Oktoba 27, 2023 Picha: AFP

Mkuu wa Kamandi ya Anga ya Jeshi la nchi hiyo Brigedia Jenerali Gilad Keinan amesema ndege zisizopungua 100 zimefanya hujuma mnamo majira ya usiku zikiyalenga mahandaki, vyumba vya chini ya majengo pamoja na miundombinu mingine ya Hamas.

Sehemu ya operesheni hiyo imehusisha pia wanajeshi wa ardhini waliotumwa kuingia Ukanda wa Gaza siku ya Ijumaa.

Hata hivyo mashambulizi hayo yamekosolewa kwa matamshi makali hii leo na rais Reccip Tayyip Erdogan wa Uturuki aliyeitaka Israel ikomeshe kile amekiita "wendawazimu" huko Gaza.

Kupitia ujumbe kwenye ukurasa wa mtandao wa X, Erdogan amesema mashambulizi ya Israel yameendelea kuwalenga wanawake, watoto na watu wasio na hatia na kutanua hali dhaifu ya kiutu kwenye Ukanda wa Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW