1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasema inaendesha operesheni za angani, ardhini Gaza

31 Oktoba 2023

Jeshi la Israel limesema askari wake wako katika mapambano makali katika Mji wa Gaza wakati likiendelea kusonga mbele kwenye operesheni yake ya ardhini dhidi ya Hamas.

Hali ilivyo kwenye Ukanda wa Gaza baada ya kushambuliwa na jeshi la Israel.
Hali ilivyo kwenye Ukanda wa Gaza baada ya kushambuliwa na jeshi la Israel.Picha: MAXAR TECHNOLOGIES via REUTERS

Msemaji wa jeshi la Israel, Daniel Hagari, alisema siku ya Jumanne (Oktoba 31) kwamba mamia ya maeneo ya Hamas yamepigwa katika mashambulizi yaliyoratibiwa ya angani na ardhini.

Soma zaidi: UNRWA: Bidhaa ya mafuta yahitajika haraka Gaza

Baada ya wiki kadhaa za msururu wa mashambulizi ya angani, jeshi la Israel lilianzisha awamu mpya ya vita vyake dhidi ya Hamas, ambao wanaudhibiti Ukanda wa Gaza, kwa kuanzisha operesheni ya mfululizo ya ardhini mwishoni mwa wiki.

Umoja wa Mataifa umesema karibu malori 100 yaliyobeba msaada yanahitajika kila siku kuwapa mahitaji ya msingi watu milioni 2.2 wanaoishi katika Ukanda wa Gaza.

Soma zaidi: Jeshi la Israel lamshambulia kiongozi wa Hamas

Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limesema uwanja wa mapambano umegeuka kuwa makaburi ya watoto.

Mpaka sasa watoto 3,400 wameshauawa Gaza katika kile ambacho Israel inasema ni kulipiza kisasi uvamizi wa Oktoba 7 uliofanywa na kundi la Hamas, ambao ulipelekea vifo vya watu wapatao 1,400 ndani ya Israel na kundi hilo kuwachukuwa mateka zaidi ya watu 200, kwa mujibu wa Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW