Israel yasema mashambulizi dhidi ya Iran kuongezeka
21 Machi 2026
Matangazo
Katz amesema hayo katika taarifa kwa njia ya video, saa chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema kuwa anafikiria kumaliza operesheni za kijeshi Mashariki ya Kati, licha ya nchi hiyo kutangaza kutuma meli zaidi za kivita na jeshi la wanamaji katika eneo hilo huku Iran ikitishia kushambulia maeneo ya utalii duniani kote.
Mapema leo, jeshi la Israel limesema limekuwa likilenga shabaha zake ndani ya Tehran.
Tangazo hilo limekuja muda mfupi baada ya jeshi hilo kusema limeanza wimbi la mashambulizi kulenga maeneo ya Hezbollah katika vitongoji vya kusini mwa Beirut nchini Lebanon.