1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasema wakosoaji wake wanawabagua Wayahudi

25 Desemba 2025

Israel imekasirishwa na ukosoaji wa mataifa 14, yakiwemo Ufaransa na Uingereza, juu ya uamuzi wake wa kuidhinisha ujenzi wa makazi mapya ya Walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu.

Israel | Gideon Saar
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gideon SaarPicha: Juan Mabromata/AFP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Gideon Saar, amesema serikali za kigeni hazina haki ya kuwazuia Wayahudi kuishi katika kile alichokiita Ardhi ya Israel, akitaja ukosoaji huo kuwa unawabagua Wayahudi.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametangaza kuwa nchi hiyo inapanga kuwekeza dola bilioni 110 katika kipindi cha miaka kumi ijayo ili kuimarisha sekta ya ndani ya utengenezaji wa silaha. Akizungumza katika hafla ya mahafali ya marubani wapya wa jeshi la anga, Netanyahu amesema mpango huo unalenga kupunguza utegemezi wa Israel kwa wauzaji wa silaha wa nje, akibainisha kuwa hata mataifa rafiki, yakiwemo Ujerumani, yataongeza ununuzi wa silaha kutoka Israel.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW