1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Askari wa Israel wajeruhiwa katika shambulio la Hezbollah

1 Julai 2024

Jeshi la Israel limeripoti jana jioni kwamba wanajeshi wake 18 wamejeruhiwa katika shambulio la ndege isiyo na rubani iliyorushwa na wanamgambo wanaoiunga mkono Iran wa Hezbollah.

Mji wa Khiam
Mji wa Lebanon wa KhiamPicha: Stringer/REUTERS

Jeshi la Israel limeripoti jana jioni kwamba wanajeshi wake 18 wamejeruhiwa katika shambulio la ndege isiyo na rubani iliyorushwa na wanamgambo wanaoiunga mkono Iran wa Hezbollah kutoka kusini mwa Lebanon kuelekea kaskazini mwa Israel.

Katika taarifa yake, jeshi la Israel limesema mmoja wa wanajeshi hao amepelekwa hospitalini akiwa na majeraha makubwa. Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa jeshi la anga la Israel lilijibu kwa kushambulia maeneo ya Hezbollah kusini mwa Lebanon.

Tangu kuanza kwa vita vya Gaza mwezi Oktoba, Israel imekuwa ikishambuliana kila siku na kundi la Hezbollah katika eneo la mpaka na Lebanon.Waziri wa ulinzi wa Israel atishia kuivuruga vibaya Lebanon

Wanamgambo hao wametangaza kuwa Israel lazima ikomeshe kabisa vita huko Gaza dhidi ya mshirika wake, kundi la Hamas, kabla ya kuacha kuishambulia Israel.