1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yasema wanamgambo 1,500 wa Hamas wameuwawa Gaza

Josephat Charo
10 Oktoba 2023

Israel imeyashambulia maeneo ya kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza hivi leo na imesema miili ya wanamgambo 1,500 imepatikana.

Jeshi la Israel limesema Jumanne kwamba wanajeshi wapatao 123 wameuwawa katika shambulizi kubwa la Hamas.
Jeshi la Israel limesema Jumanne kwamba wanajeshi wapatao 123 wameuawa katika shambulizi kubwa la Hamas.Picha: Ronen Zvulun/REUTERS

Miili hiyo imepatikana katika miji ya kusini iliyokombolewa na jeshi katika mapambano makali karibu na eneo hilo la Palestina.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametahadharisha kwamba kampeni ya kijeshi ya Israel kufuatia mashambuli ya Jumamosi iliyopita ni mwanzo wa vita virefu vya kuiangamiza Hamas na kuibadili Mashariki ya Kati.

Idadi ya vifo nchini Israel imevuka 900 kufuatia shambulizi baya kabisa katika historia ya miaka 75 ya taifa hilo, huku maafisa wa Gaza wakiripoti kuwa watu 687 wameuliwa kufikia sasa.

Jeshi la Israel limesema Jumanne kwamba wanajeshi wapatao 123 wameuwawa katika shambulizi kubwa la Hamas.

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kutoa kauli kuhusu hali nchini Israel baadaye Jumanne.

Umoja wa Mataifa unasema watu karibu 200,000 wameyakimbia makazi yao huko Gaza tangu vita kuzuka na uhaba wa maji na ukosefu wa umeme unatarajiwa kufuatia kuzingwa kwa eneo hilo.