1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel yashambulia Gaza baada ya shambulio la roketi

2 Februari 2023

Jeshi la Israel limesema vikosi vyake vimeshambulia maeneo katika Ukanda wa Gaza, kujibu shambulio la roketi kutoka eneo hilo.

Gaza | Israelische Luftangriffe auf Gaza
Picha: Fatima Shbair/AP/picture alliance

Jeshi la Israel limesema vikosi vyake vimeshambulia maeneo katika Ukanda wa Gaza, kujibu shambulio la roketi kutoka eneo hilo.

Katika taarifa yake kupitia mtandao wa Twitter, jeshi hilo la IDF limesema mashambulizi yake yalilenga kituo cha uzalishaji wa kemikali ghafi, pamoja na kituo cha utengenezaji silaha, ambacho limesema kinamilikiwa na kundi la Hamas linalodhibiti ukanda huo.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari ambazo hazijathibitishwa, ndege za kivita za Israel zilishambulia maeneo kwenye kambi ya wakimbizi katikati mwa Gaza. Masaa machache kabla ya shambulio la Israel, jeshi lilisema lilikuwa limezuwia roketi kutoka Ukanda wa Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW