1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia Gaza

9 Januari 2008

GAZA:

Saa chache kabla ya rais Bush kuwasili katika eneo la mashariki ya kati, vikosi vya Israel vimevurimisha kombora katika maeneo ya kaskazini mwa ukanda wa Gaza.

Kombora hilo limemuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine 6, wawili wakiwa wamejeruhiwa vibaya. Msemaji wa jeshi la Israel amesema kuwa jeshi limeshambulia alichokiita,mtambo wa kufyatulia roketi katika eneo la Beit Lahiya, baada ya wanamgambo kufyatua maroketi kadhaa nchini Israel.