1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Israel yashambulia kambi za ulinzi nchini Syria

Josephat Charo
30 Julai 2024

Shirika linalofuatilia masuala ya haki za binadamu la Syria limesema mashambulizi ya Israel yamezipiga kambi za ulinzi kusini mwa Syria usiku wa kuamkia leo.

Syria yashambulia jengo karibu na ubalozi wa Iran mjini Damascus
Shambulio la Syria kwenye jengo moja karibu na ubalozi wa Irani huko Damascus huko Damascus, Syria Aprili 1, 2024. Picha: Firas Makdesi/REUTERS

Hayo yanatokea wakati hali ya wasiwasi ikiongezeka katika mpaka wa kaskazini wa Israel kufuatia shambulizi lililosababisha vifo katika milima ya Golan. Shirika hilo halikuripoti maafa wala majeruhi yoyote katika mashambulizi hayo ya usiku kucha katika mkoa wa Daraa, ulioko katika eneo linalovitenganisha vikosi vya Syria na Israel katika milima ya Golan. Chombo cha habari ya serikali ya Syria hakikuripoti mashambulizi yoyote. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Naetanyahuameapa kuchukua hatua kali kujibu shambulizi la Jumamosi iliyopita lililowaua vijana 12 katika mji wa jamii ya kiarabu ya Druze katika milima ya Golan. Viongozi wa jamii hiyo wamesema hivi leo wamejitenga na kitisho hicho cha Israel kutaka kulipiza kisasi dhidi ya kundi la Hezbollah nchini Lebanon kwa shambulizi hilo la umwagaji damu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW