1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia karibu maeneo 300 ya Hezbollah

22 Oktoba 2024

Israel imesema imeshambulia karibu maeneo 300 ya Hezbollah nchini Lebanon kwa muda wa saa 24 zilizopita, na kuvilenga zaidi vyanzo vinavyolifadhili kundi hilo.

Jengo la Kampuni ya kifedha ya Al-Qard al-Hassan kusini mwa mji wa Beirut.
Jengo la Kampuni ya kifedha ya Al-Qard al-Hassan kusini mwa mji wa Beirut.Picha: Mohamed Azakir/REUTERS

Jeshi la Israel limesema miongoni mwa maeneo 30 yenye mafungamano na Hezbollah yaliyoshambuliwa ni pamoja na handaki lenye dhahabu na mamilioni ya dola lililokuwa likimilikiwa na kampuni ya kifedha ya Al-Qard al-Hassan kusini mwa mji wa Beirut.

Soma pia: Wanamgambo wa Hezbollah wadai kuvishambulia vikosi vya Israel

Umoja wa Mataifa umelaani mashambulizi hayo na kuyataja kuwa "uharibifu wa mali za kiraia". Marekani na Umoja wa Nchi za Kiarabu wametoa wito wa kusitisha mara moja mapigano nchini Lebanon na kufufua mchakato wa mazungumzo wa kumaliza mzozo wa Gaza na Lebanon.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW