1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia katikati ya Gaza, yaingia ndani Rafah

20 Juni 2024

Majeshi ya Israel yameyashambulia maeneo ya katikati mwa Ukanda wa Gaza na kuwaua watu watatu.

Vita vya Israel na Hamas
Israel imeendelea kuzipiga kambi za wakimbizi katikati ya Gaza na kusonga ndani zaidi ya RafahPicha: Ahmed Ibrahim/APA/ZUMA/picture alliance

Watu wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulio hayo ya usiku wa kuamkia Alhamisi. Ndege za Israel pia ziliishambulia kambi ya AL-Nuseirat na kumuua mtu mmoja. Watu wengine 12 wamejeruhiwa.

Soma pia: Msemaji wa jeshi la Israel asema Hamas haiwezi kusambaratishwa

Taarifa hiyo imetolewa na wahudumu wa hospitali ya Gaza. Vifaru vya Israel pia vilishambulia kwa mizinga kwenye kambi za Al-Maghazi na Al-Bureji. Kambi hizo ni za kihistoria kwenye Ukanda wa Gaza.

Soma pia: Netanyahu avunja Baraza lake la vita nchini Israel

Jeshi la Israel limesema vikosi vyake vinaendelea na operesheni katika eneo hilo kuwalenga wanamgambo wa Hamas na kuiharibu miundombinu yao ya kijeshi katika hatua ambayo jeshi la Israel limesema ni sahihi, na inafanyika kutokana na taarifa za intelijensia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW