1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yashambulia kitongoji kimoja kusini mwa Beirut

1 Novemba 2024

Israel imevishambulia vitongoji vya kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut kwa mfululizo wa mashambulizi ya angani mapema leo. Ni mashambulizi ya kwanza ya aina hiyo kufanywa katika siku za karibuni.

Moshi ukionekana kutokana na mashambulizi ya Israel huko Beirut
Moshi ukionekana kutokana na mashambulizi ya Israel huko BeirutPicha: Kawnat Haju/AFP

Israel imevishambulia vitongoji vya kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut kwa mfululizo wa mashambulizi ya angani mapema leo. Hii ni baada ya kutoa maagizo ya kuwataka wakaazi wahame. Ni mashambulizi ya kwanza ya aina hiyo kufanywa katika siku za karibuni yanayolilenga eneo hilo lenye idadi kubwa ya watu. Israel na Hezbollah zashambuliana kwenye maeneo muhimu

Jeshi la Israel limesema lilivilenga vituo na mali za Hezbollah. Mashambulizi hayo yamefuatia juhudi ambazo mpaka sasa hazijafua dafu za kidiplomasia zinazoongozwa na Marekani zikililenga kupata muafaka wa kusitishwa mapigano Gaza na Lebanon kati ya Israel na makundi yanayoungwa mkono na Iran ya Hamas na Hezbollah.Israel yauwa 28 Gaza, 3 Lebanon

Wakati huo huo, Wapalestina 47 wameuawa na wengine wamejeruhiwa, wengi wao watoto na wanawake, katika mashambulizi ya usiku kucha ya Israel katikati mwa Ukanda wa Gaza. Shirika la Habari la Kipalestina WAFA limesema mashambulizi hayo yalifanywa katika mji wa Deir Al-Balah, kambi ya wakimbizi ya Nuseirat na mji wa Al-Zawayda. Jeshi la Israel limesema askari wake waliwaangamiza magaidi kadhaa wenye silaha katikati ya Gaza na wengine katika eneo la Jabalia kaskazini mwa Ukanda huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW